Duration 31:8

MAKALA MAALUMU: Wizara ya kilimo yaanisha mafanikio siku 100 za Rais Samia

178 watched
0
0
Published 4 Jul 2021

WAZIRI wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda anasema wakati akilihutubia bunge kwa mara ya kwanza Rais wa Awamu ya sita Samia Suluhu Hassan alitumia takribani asilimia 14 ya mambo yote aliyozungumza kwenye masuala ya kilimo. Hayo aliyabainisha hivi karibuni wakati akitoa maelezo kuhusu siku 100 za Rais Samia akiwa madarakani tangu kifo cha Rais wa awamu ya tano, Hayati Rais John Magufuli kitokee. Waziri huyo anasema jambo moja ambalo Rais, alilitamka ni umuhimu wa kuongeza tija katika kilimo kwakuwa bila kufanya hivyo nchi inaweza isiende vizuri kwenye sekta hiyo. Alitolea mfano kuwa sasa hivi kwenye kahawa uzalishaji unaweza kuongezwa tija mara tatu ya kahawa inayozalishwa kwa sasa licha ya kuwa kwa sasa tija ni ndogo hivyo kupatikana theluthi tuu ya uzalishaji. Amesema kwa upande wa Pamba kwenye hekari moja unapata takribani kilo 200 mpaka 350 lakini kwa nchi nyingine za Afrika Magharibi wanapata mpaka kilo 1000 hivyo tija bado ni ndogo. ”Bila hata kuongeza eneo la kulima tunaweza tukaongeza uzalishaji hivyo ukienda zao moja hadi jingine unakuta kwamba tija ni ndogo sana” Amesema Anasema Rais Samia alielekeza nguvu kubwa ielekezwe katika kuongeza tija hivyo bajeti ya wizara ya Kilimo iliyosomwa bungeni imeanisha mikakati ya kuongeza tija na fedha katika maeneo ya kupaumbele. Anaeleza waliona cha muhimu katika yote ni suala la utafiti wa mbegu bora ambazo zinaongeza tija, na kilimo bora. Amesema hayo ni mafanikio makubwa kwa sababu alitembelea baadhi ya vituo vya utafiti ambavyo watu wameanza kukata tamaa na kuhisi kwamba serikali ilikuwa ikipuuza suala hilokwa sababu hautoi matokeo mara moja hali inayosababisha watu kutafuta vitu vyenye matokeo ya haraka. Alisema suala la pili ni kuzalisha mbegu bora zaidi kutokana na uhaba wake kuwa ni kikwazo kikubwa cha uzalishaji wa tija huku akitolea mfano zao la alizeti ambalo kwa sasa serikali imekusudia kuongeza wazalishaji nchini licha ya kutokuwepo mbegu. ”Tumeamua mashamba yote ya mawakala wa mbegu Tanzania 13 tutayafufua, kuyamawagilia ili yaanze kuzalisha mbegu ziwafikie wakulima na tumeongeza bajeti kubwa kwenye suala la uzalishaji wa mbegu,” Alisema. Alifafanua kuwa bajeti imeongezwa kwenye huduma ya ugani ambayo ilikuwa milioni 603 tuu hadi bilioni 11.5 licha ya kuwa hazitoshi hivyo nguvu itawekwa mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu kuonyesha namna huduma hiyo inatakiwa ifanyike ili kuongeza tija. Pia, alisema utaanzishwa mfuko wa umwagiliaji kwa ajili ya kuhakikisha kwamba uzalishaji wa ekari unaongezeka. Alieleza pamoja na mambo hayo kuna masuala ya masoko ili kuhakikisha kwamba mkulima anapolima anaweza kuuza huku akieleza tatizo lipo la aina mbili ambapo ni uzalishaji ambao wakulima hawajui wauze wapi bidhaa zao.

Category

Show more

Comments - 0